Dodoma FM

Elimu ya afya ya uzazi inawasaidiaje mabinti kuepuka mimba za utotoni?

28 May 2026, 18:02

Hii ni hatua muhimu katika kukabiliana na changamoto hii inayowakumba mamilioni ya wasichana duniani.​Picha na WHO.

Pia, unalenga kushughulikia vikwazo vya kijamii na kisheria vinavyowazuia wasichana kupata huduma za afya ya uzazi.

Na Mariam Kasawa.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni WHO limetoa mwongozo mpya wa kimataifa unaolenga kuzuia mimba za utotoni na kuboresha afya za wasichana, likiwa ni hatua muhimu katika kukabiliana na changamoto hii inayowakumba mamilioni ya wasichana duniani.​

Mwongozo huu mpya wa WHO unasisitiza umuhimu wa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana, upatikanaji wa huduma rafiki kwa vijana, na usaidizi kwa wasichana waliopata mimba au walioolewa wakiwa watoto.