Dodoma FM

Wakazi Mkoani Dodoma walalamikia kukosa taarifa juu ya mikopo ya asilimia kumi

16 August 2021, 1:44 pm

Na;Yussuph Hans.

Wakazi mkoani Dodoma wamelalamikia kukosa taarifa juu fursa ya mikopo ya asilimia kumi inayotolewa na kila halmashauri nchini kwa vikundi vilivyosajiliwa vya vijana, wanawake na Watu wenye ulemavu.

Wakizungumza na kitu hiki wakazi hao wamesema kuwa wanapata changamoto kubwa ya taarifa juu ya mikopo hiyo suala ambalo linawawia vigumu kuchangamkia fursa hizo.

Aidha wameshauri serikali kutoa mikopo hiyo kwa mtu binafsi kuliko ilivyosasa mikopo inatolewa kwa vikundi hali ambayo inasababisha changamoto baadhi ya muda katika marejesho.

Kwa upande wake afisa maendeleo kwa vijana jijini dodoma mfungo manyama amesema kuwa taarifa zimekuwa zikitolewa katika vyombo vya habari na ofisi za kiserikali katika kila wilaya hivyo vyema jamii ikawa na utaratibu wa kufatilia taarifa hizo.

Katika hatua ameshauri jamii kuchamkia mikopo ya halmashauri ambayo haina riba katika kuboresha uchumi wao kupitia miradi mbalimbali.

Ni wajibu uliowekwa na sheria kwa Serikali za Mitaa kutenga asilimia kumi ya mapato yanayokusanywa kutoka kwenye vyanzo vya ndani vya mapato kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vikundi vilivyosajiliwa vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.