Dodoma FM

Rais Samia ateua, atengua Mkurugenzi ndani ya saa 12

6 April 2021, 7:01 am

Na; Mariam Kasawa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya petroli Tanzania (TPDC), Thobias Richard ikiwa ni chini ya masaa 24 tangu kuteuliwa kwake.

Rais Samia alimteua Richard miongoni mwa wakuu wa mashirika alio wateua lakini leo asubuhi ametengua uteuzi huo na kumrejesha Dkt. James Mataragio kuendelea kuwa Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo.

Dkt. Mataragio ndiye alikuwa Mkurugenzi wa shirika hilo kabla ya uteuzi wa Richard na kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya mawasiliano ya Rais Ikulu Dk Mataragio anaendelea na majukumu yake mara moja.

Aidha taarifa hiyo iliyotolewa  jana  asubuhi Aprili 5, 2021 inaeleza kuwa uapisho wa viongozi walioteuliwa jana utafanyika leo Aprili 6, saa 4 kamili asubuhi Ikulu jijini Dar es Salaam.