Dodoma FM

Waziri Ummy aitaka Mirembe kujikita katika kukuza afya ya akili

19 April 2023, 12:42 pm

Waziri wa Afya mh. Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo. Picha na wizara ya Afya.

Kituo hicho kitahusisha huduma za tiba ya akili, tafiti mbalimbali za maradhi hayo, mafunzo ya Afya za akili na kuhamasisha jamii kuwa na uelewa juu ya Afya ya akili.

Na Alfred Bulahya

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu  ameitaka  Bodi ya Ushauri ya Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe kujikita katika masuala ya kukuza Afya ya akili ikiwa ndiyo lengo mahususi la kuanzishwa hospitali hiyo.

Mhe. Ummy ametoa wito huo Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Bodi  Mpya ya Ushauri ya Hospitali ambapo amesema kuwa Hospitali hiyo inatakiwa kuwa kituo mahiri cha masuala ya Afya ya akili nchini.

Akizungumza Mhe. Ummy amesema kituo hicho kitahusisha huduma za tiba ya akili, tafiti mbalimbali za maradhi hayo, mafunzo ya Afya za akili na kuhamasisha jamii kuwa na uelewa juu ya Afya ya akili.

Sauti ya Waziri wa Afya