Dodoma FM

Biashara ya chakula jijini Dodoma yashuka

28 March 2023, 1:42 pm

Ugumu wa biashara hususani katika kipindi hiki ambapo waislamu na baadhi ya wakristo wakiwa katika kipindi cha mfungo.Picha na Martha Mgaya

Wafanyabiashara wa vyakula jijini Dodoma wamelalamikia ugumu wa biashara hususani katika kipindi hiki ambapo waislamu na baadhi ya wakristo wakiwa katika kipindi cha mfungo.

Na Thadei Tesha.

Wafanyabiashara wa vyakula jijini Dodoma wamelalamikia ugumu wa biashara hususani katika kipindi hiki ambapo waislamu na wakristo wakiwa katika kipindi cha mfungo.

Dodoma FM imewatembelea wafanyabiashara wa chakula na nimeanza kwa kuwauliza mwenendo wa biashara hiyo.

Sauti za wafanyabiashara.

Wananchi jijini Dodoma wanasema katika kipindi cha mfungo kama hiki baadhi ya waumini hujinyima chakula kama ishara ya kujutia na kuomba kusamehewa makosa yao kwa mwenyezi Mungu hivyo kutokutumia chakula kwa siku.

Sauti z wananchi.

Waumini wa dini ya kikristo pamoja na waislamu kote duniani wapo katika mfungo wa mwezi mtakatifu wa ramadhani pamoja na kipindi cha kwaresma jambo linalosababisha wengi wao kujinyima chakula kama ishara ya kutimiza taratibu za dini hizo.