Dodoma FM

Wakazi jijini Dodoma wamehamasishwa kujiunga na Bank ya Amana.

11 May 2021, 10:54 am

Na; Mariam Kasawa.

Wakazi jijini Dodoma wamehamasishwa kufungua akaunt katika Bank  ya Amana kwani ni nafuu na rahisi kutoa huduma kwa jamii.

Akizungumza na kapu kubwa la Dodoma fm meneja wa bank ya Amana tawi la Dodoma Bw. Athuman Julius amesema  Amana Bank inawakaribisha watu mbalimbali kufungua accout kwa kuambatanisha nakala zinazo takiwa wakati wa kufungua account ikiwemo kitambulisho cha Taifa ,au cha  kupiga kura, leseni ya udereva , picha moja au barua kutoka kwa mwenyekiti wa mtaa pamoja na pesa ya kufungulia account.

Amesema amana Bank inazo account za aina mbalimbali ikiwemo ya watoto wadogo  hadi watu wazima.

Adha amesema kupitia Card ya Amana Bank Master Card unaweza kulipia bidhaa kupitia ATM yeyote iliyopo karibu yako yenye huduma ya master card.