Dodoma FM

Uhaba wa wachangia Figo waendelea kuwa kikwazo

13 March 2023, 5:49 pm

Mkurungezi Mtendaji wa Hospital ya Benjamin Mkapa Dkt Alphonce Chandika.Picha na Habari Maelezo.

Mpaka sasa Hospitali ya Benjamin Mkapa imefanikiwa kupandikiza Figo  wagonjwa 33 kati ya hao wagonjwa 22 walipandikizwa Figo na wataalamu wazawa.

Na Mindi Joseph.

Ukosefu wa wachangiaji  Figo  umetajwa kuendelea kuwa kikwazo kwani Wananchi wengi hawapo tayari kujitolea kuchangia Ndugu zao.

Hayo yamebainishwa Leo Mkurungezi Mtendaji wa Hospital ya Benjamin Mkapa Dkt Alphonce Chandika katika maadhimisho ya miaka 5 ya upandikizaji Figo katika Hospital hiyo.

Amesema katika miaka mitano wamegundua kuwa wananchi hawapo tayari kuchangia Figo.

Sauti ya Mkurungezi Mtendaji wa Hospital ya Benjamin Mkapa Dkt Alphonce Chandika

Kwa upande wake Neema Sweti Mkazi wa ihumwa Jijini Dodoma anaeleza ilivyojitolea kuchangia Figo huku Faraji Shaban aliyefanikiwa kupandikizwa Figo akaipongeza serikali

Sauti za Wananchi.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, UDOM, Prof. Lughano Kusiluka naye amesema.

Sauti ya Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, UDOM, Prof. Lughano Kusiluka .