Dodoma FM

Billioni 12 zatarajiwa kutekeleza miradi ya barabara Bahi

28 July 2023, 2:13 pm

Wananchi wa kijiji cha Bahi Sokoni wakiwa kwenye mkutano wa hadhara.Picha na Bernadi Magawa.

Kupitia mradi huo wananchi wametakiwa kuanzisha miradi midogomidogo itakayowasaidia kujikwamua kimaisha.

Na.  Bernad Magawa

Zaidi ya Shilingi Billion 12 zinatarajiwa kutekeleza miradi ya barabara wilayani Bahi mwaka huu ili kuboresha miundombinu ya usafiri na kuharakisha maendeleo ya wananchi wa Bahi.

Hayo yamesemwa na diwani wa kata ya Bahi Mheshimiwa Agostino Ndonu alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Bahi Sokoni kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo Julai  26 mwaka huu huku akiwasisitiza wananchi kuanzisha miradi midogomidogo ya kujiongezea kipato.

Sauti ya Diwani wa kata ya Bahi .

Nao  baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo walipata nafasi ya kueleza kero mbalimbali zinazowakabili ili ziweze kutafutiwa ufumbuzi ambapo suala la mifugo kuharibu mashamba ya mpunga likaibuka.

Sauti za wananchi.
Wananchi wa kijiji cha Bahi sokoni wakiwa kwenye mkutano wa hadhara.Picha na Bernadi Magawa.

Akijibu baadhi ya hoja hizo, Afisa Mtendeji wa kata ya Bahi Agostino Kizungo amewashauri wananchi kujiunga na bima ya afya ili kuondokana na matumizi ya fedha wanapokwenda kupata huduma za afya huku afisa kilimo wa kata hiyo Catherine  Ipemba akikemea vikali wafugaji wanaoharibu mashamba ya mpunga na kueleza kuwa mifungo kuharibu mashamba faini yake ni shilling millioni moja au kifungo jela miezi 6.

Sauti ya Afisa Mtendaji kata ya Bahi.