Dodoma FM

Madereva kirikuu walalamika kutozwa faini mara kwa mara

20 February 2023, 6:09 pm

Gari ndogo za kubeba mizigo jijini Dodoma maarufu kama Kirikuu. Picha na Thadey Tesha.

Gari ndogo aina ya kirikuu zimekuwa zikifanya shughuli zao katika maeneo mbalimbali jijini hapa ambapo shughuli hiyo imekuwa ikiwasaidia kwa kiasi kikubwa katika kupata fursa mbalimbali na kuendesha shughuli zao za kimaisha.

Na Thadei Tesha.

Madereva wa gari ndogo za  mizigo maarufu kama kirikuu wamelalamikia baadhi ya tabia za askari wa usalama barabarani kuwatoza faini za mara kwa mara pale wanapokuwa katika majukumu yao ya kubeba mizigo ambapo wamesema kuwa kufanya hivyo kumewapelekea wao kupata hasara.

Dodoma FM imefanya mahojiano na baadhi ya madereva wa gari hizo jijini dodoma ambapo wamesema kuwa askari wa usalama barabarani jijini hapa wamekuwa wakiwakamata  na kuwatoza faini mara kwa mara ambapo wamesema kwa kufanya hivyo kunawapelekea kushindwa kupata faida katika shughuli zao.

Sauti ya Madereva.

Akizungumzia suala hilo mrakibu msaidizi wa jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Dodoma Insepekta Bwigam  Mwakatobe amesema wamekuwa wakiwakamata madereva hao kutokana na makosa mbalimbali ambapo wapo baadhi yao ambao wamekuwa wakibeba mizigo kinyume na utaratibu.

Sauti ya Mrakibu msaidizi Insepekta Bwigam  Mwakatobe.