Dodoma FM

Wakazi wa Chamwino waahidi kuziishi ndoto za Rais Magufuli

26 March 2021, 10:29 am

Na Selemani Kodima

Mkuu wa wilaya ya Chamwino Vumilia Nyamoga amesema wataendelea kumkumbuka Hayati Magufuli kwa Juhudi zake ambazo alizionesha kwa wakazi wa Chamwino katika Huduma za Msingi ikiwemo Huduma ya Maji na umeme.

Bi Nyamoga amesema Hayati Magufuli alionyesha kuwathamini wakazi wa Chamwino pale ambao alitoa Agizo kwa RUWASA kusambaza huduma ya maji wananchi wa wilaya hiyo ili waweze kufaidika na maji kama ambavyo yalikuwa yanapatikana Ikulu ya Chamwino bila shida yoyote.

Amesema Maisha ya Hayati Magufuli aliyajenga kwa  kutembelea wananchi na kuzungumza nao na kuonesha mchango wake katika wilaya ya Chamwino.

Bi Nyamoga amesema kutokana na Juhudi za Hayati Magufuli katika kuifanya wilaya ya Chamwino kukua kila Nyanja wataenzi yale yote  yaliyo kuwa matamanio yake katika wilaya hiyo kama Usalama,Umoja pamoja na kulinda Miundombinu ya Taasisi mbalimbali ndani ya Wilaya ya Chamwino.

Pamoja hayo amesema wananchi wa wilaya ya Chamwino wameguswa na Msiba wa Rais Magufuli kutokana kiongozi huyo kuwa mstari wa mbele katika kuitetea Wilaya ya  Chamwino pamoja na Mkoa wa Dodoma .