Dodoma FM

Wafanyabiashara Dodoma Wamshukuru Magufuli

24 March 2021, 1:14 pm

Na; Shani  nicholous .

Kufuatia kifo cha aliyekuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hayati Dkt.John Magufuli bado wajasiriamali wadogo pamoja na wafanyabiashara mbalimbali wameendelea kumlilia na kumshukuru kwa kuwaboreshea mazingira yao ya biashara.

Wakizungumza na Dodoma Fm wajasiriamali hao wanaouza bidhaa za asili wamesema kuwa hayati Dkt.Mgufuli aliwawezesha kufanya biashara zao kwa uhuru na kuwatetea wakati wote walipoonewa.

Aidha wamesema kuwa wanataraji mazuri kutoka kwa Rais mpya Mh.Samia Suluhu Hassani kwani hakuna asichokifahamu Serikalini kutokana na kufanya kazi kwa muda mrefu, hivyo wanaomba afuate nyayo za uongozi wa hayati Magufuli.

Hata hivyo, jamii ya wafugaji imeomba bei ya mifugo itiliwe mkazo ili kuleta tija katika ufugaji kuliko kufuga kwa mazoea.