Dodoma FM

Baraza la Taifa la mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali NaCoNGO latangaza rasmi viongozi wapya

9 July 2021, 11:07 am

Na; Mindi Joseph.

Baraza la Taifa la Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali (NaCoNGO) limetangaza rasmi viongozi wapya waliochaguliwa nafasi za ngazi ya kitaifa watakaoongoza kwa kipindi cha miaka mitatu.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo,Julai 8,2021,Mwenyekiti wa Kamati ya mpito iliyosimamia uchaguzi huo,Flaviana Charles amemtaja Mwenyekiti mpya wa Baraza hilo, kuwa ni Lilian Badi huku Katibu Mkuu ni Revocatus Sono kwa kura 22 Nafasi ya Mwekahazina wajumbe hao wamemchagua John Kiteve kwa kura 15 nafasi ya Kamati ya Fedha na Utawala wamempigia kura za ndio Gaidon Haule ambaye alikuwa peke yake katika nafasi hiyo.

Katika kamati ya maadili wajumbe hao wamemchagua Novatus Marandu ambaye amepata kura 15 na Kamati ya Maendeleo na Uwezo akichaguliwa Rhobi Samweli,Kamati ya Utandaa na Mawasiliamo akichaguliwa Asifiwe Mallya huku wajumbe wanne wa Bodi wakiwa ni Jane Magigita,Revocatus Sono,Paulina Majogoro na Baltazari Komba.

Mjumbe wa kamati ya mpito iliyoteuliwa na Waziri wa Afya kuhusu uchaguzi ,Yasin Ally amesema uwepo wa baraza hilo itasaidia kuratibu kikamilifu mchango wa mashirika yasiyo ya kiserikali .

Akizungumza mara baada ya kutangazwa kwa matokeo Mwenyekiti mpya Baraza hilo,Lilian Badi ameomba ushirikiano huku akiahidi kutekeleza yale ambayo aliahidi wakati wa kuomba kura.

Kwa upande wake,Katibu mpya wa Baraza hilo, Revocatus Sono amewashukuru wote waliomwamini kwa kumpigia kura ambapo amedai kwamba mchakato huo haukuwa mdogo.

Ikumbukwe kuwa kufanyika kwa uchaguzi huo imetokana na agizo la Waziri wa Afya ,maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee Dkt.Dorothy Gwajima alilolitoa hivi karibuni kwa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali (NaCoNGO)kufanya uchaguzi kama ivyo kwa mujibu wa sheria ya baraza la mashirika yasiyo ya kiserikali ambapo inaelekeza kufanyika uchaguzi kila baada ya miaka mitatu