Dodoma FM

Mitaro inayopitisha maji yakwamisha shughuli za wakazi wa Ihumwa A

11 January 2024, 6:34 pm

Serikali imeombwa kuchukua hatua za haraka kwa kujenga vivuko vitatu ili kutatua changamoto hiyo katika mtaa huo,Picha na Google.

Ni miaka miwili sasa Wananchi wa Mtaa wa Ihumwa A jijini Dodoma wanalalamikia mchangamoto hiyo licha ya juhudi kubwa iliyofanywa mwaka jana na kampuni ya Ujenzi wa Reli ya Kisasa ya Yap Markez kuchimba mtaro huo.

Na Victor Chigwada.
Wakazi wa mtaa wa Ihumwa A jijini Dodoma wamelalamika kupata kero kutokana na kukosekana kwa Vivuko kwenye baadhi ya Mitaro inayopitisha maji na kusababisha shughuli zao kusimama pindi maji yanapozidi kwenye mitaro hiyo.

Hayo wameyasema wakati wakizungumza na Taswira ya Habari kuhusu kukosekana kwa Vivuko kwenye mitaro ndani ya mtaa huo.

Sauti za wananchi wa Ihumwa A.

Baadhi ya wananchi hao wamesema changamoto hiyo imesababisha kuongezeka gharama za usafiri kutoka eneo moja kwenda lingine huku sababu ikiwa ni kukwepa adha hiyo inayo hatarisha usalama wao.

Sauti za wananchi wa Ihumwa A.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa huo Bw.Wiliamu Njilimuyi amekiri uwepo wa changamoto hiyo ambapo amesema tayari yupo mkandarasi ambaye ameendelea kushughulikia changamoto hiyo licha ya mwenendo wa ujenzi wake kutoridhisha.

Sauti ya Bw.Wiliamu Njilimuyi .

Njilimuyi ameiomba Serikali kuchukua hatua za haraka kwa kujenga vivuko vitatu ili kutatua changamoto hiyo katika mtaa huo.

Sauti ya Bw.Wiliamu Njilimuyi .