Dodoma FM

Wananchi wakosa elimu ya mboga lishe

17 April 2023, 4:50 pm

Aina mbalimbali ya mboga lishe katika soko la Majengo jijini Dodoma. Picha na Thadei Tesha.

Mboga lishe ni miongoni mwa bidhaa za mbogamboga zinazopatikana katika masoko mbalimbali jijini Dodoma ingawa bidhaa hii imekuwa ikipatikana kwa uchache .

Na Thadei Tesha.

Baadhi ya wafanyabiashara wa mboga lishe jijini Dodoma wamesema kuwa ukosefu wa elimu pamoja na uchache wa bidhaa hizo sokoni kunapelekea watu wengi kuto nunua bidhaa hiyo hivyo kupelekea kutokupata wateja kwa kiasi kikubwa.

Hayo yamesemwa na baadhi ya wafanyabiashara wa bidhaa hiyo katika soko kuu la majengo jijini hapa ambapo kwanza wanaanza kwa kuelezea hali ya biashara hiyo iliovyo kwa sasa sokoni hapo.

Sauti za wafanyabishara.
Mfanyabiashara wa mboga lishe katika soko la Majengo jijini Dodoma .picha na Thadei Tesha.

Aidha Dodoma tv imefanya mahojino na baadhi ya wananchi jijini hapa kuhusiana na ni kwa kiasi gani wanazifahamu mboga lishe nao wakawa na haya ya kuzungumza.

Sauti za wanunuzi.