Dodoma FM

Waiomba Serikali kuwatengenezea mazingira rafiki

22 December 2020, 12:23 pm

Na,Thadey Tesha,

Dodoma

Baadhi ya wafanyabiashara wa kuku katika soko la Changombe jijini hapa wameiomba  Serikali kuwatengenezea mazingira rafiki ya kuuzia bidhaa zao kutokana na eneo lililopo kutotosheleza mahitaji.

Wakizungumza na Taswira ya habari wafanyabiashara hao wamesema kwa sasa mazingira wanayofanyia biashara hiyo sio rafiki kutokana na eneo hilo kuwa dogo huku wakiiomba Serikali kuwapatia mikopo yenye riba nafuu ili waweze kukuza biashara hiyo.

Aidha wafanyabiashara hao wametoa wito kwa wateja kujitokeza kwa wingi kwa lengo la kununua bidhaa hiyo kwa ajili ya msimu wa sikukuu kwani bidhaa hiyo inapatikana kwa bei nafuu.