Dodoma FM

Ishi na mti kauli njema ya kutunza mazingira

5 April 2023, 5:16 pm

Meneja wa Dodoma media group akikagua miti iliyopandwa na Dodoma sekondary Kampeni ya ISHI NA MTI .Picha na Fred Cheti.

Kampeni ya ISHI NA MTI ni kampeni iliyoanzishwa na Kampuni ya Dodoma Media Group kwa lengo la kuunga mkono juhudi za serikali katika utunzaji wa Mazingira hasa upandaji wa miti katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dodoma.

Na Fred Cheti.

Wananchi mkoani Dodoma wamehimizwa kuendelea kutunza mazingira ikiwemo kuithamini na kuitunza miti inayopandwa na serikali, taasisi pamoja na wadau mbalimbali wa mazingira.

Wito huo umetolewa na Meneja wa Kampuni ya Dodoma Media Group Bi. Zania Miraji alipotembelea kujua maendeleo ya miti iliyopandwa na wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa kushirikiana na halmashauri ya jiji la Dodoma katika eneo la Shule ya Sekondari Dodoma Ikiwa ni sehemu ya kampeni ya  ISHI na MTI inayotekelezwa na dodoma media group.

Sauti ya meneja wa DMG

Baadhi ya maeneo ambayo miti hiyo ilipandwa imeonekana kufa kutokana na shughuli za kibinadamu ikiwa ni pamoja na uwepo wa kituo cha bajaji katika eneo hilo ambapo medereva waliopo katika kituo hicho wameahidi kupanda miti eneo hilo ili kufidia miti iliyokufa.

Sauti za madereva
Moja kati ya miti iliyopandwa katika eneo hilo ikiendelea kumea.Picha na Fred Cheti.

Bwn. Paulo Mpandiko ni Katibu wa Mazingira katika shule ya sekondari Dodoma ambao ndio wasimamizi wakubwa wa miti hiyo hapa aneleza maendeleo ya miti hiyo pamoja na mikakati ya shule katika kuilinda.

Sauti ya Katibu wa Mazingira katika shule ya sekondari Dodoma