Dkt.Gwajima:Wanaume vunjeni ukimya
2 February 2021, 1:58 pm
Na,Seleman Kodima,
Dodoma.
Wahanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia wametakiwa kuacha kujificha bali kujitokeza na kutoa taarifa ili Vitendo hivyo viweze kudhibitiwa kwa haraka na kusaidia kukabiliana navyo.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Dorothy Gwajima, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii, ambapo amesema wajibu wa kamati za amani katika ngazi ya Vijiji na Mitaa ni pamoja na viongozi kufanyia kazi matukio ya ukatili wa kijinsia.
Aidha Dkt.Gwajima ametoa wito kwa maafisa ustawi wa jamii wa Halmashauri kote nchini kusimamia utekelezaji wa maagizo, ambayo ameyatoa Januari 29 kuhusu kudhibiti masuala ya ukatili dhidi ya Wanawake ,wanaume ,Watoto na Wazee.
Kwa upande mwingine amewataka wanaume kutokaa kimya juu ya Vitendo vya ukatili ambavyo wamekuwa wakifanyiwa, badala yake watoe taarifa kwa idara zinazohusika .