Dodoma FM

Waziri Gwajia awataka wazazi kuwajibika ipasavyo katika malezi ya familia zao

27 August 2021, 10:58 am

Na; Mariam Matundu.

Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dkt. Doroth Gwajima amekemea wazazi wanaochangia uwepo wa watoto wa mitaani na wanaoishi kwenye maingira magumu kwa kuwa wameshindwa kuwajibika ipasavyo katika malezi ya familia zao.

Hayo yamebainishwa jijini Dodoma yalipo makao ya taifa ya kulelea watoto kikombo Mara baada ya kamati ya kudumu ya bunge ya huduma na maendeleo ya jamii kutembelea kituo hicho kwa lengo la kuangalia uendeshwaji wa kituo hicho ambapo amesema kuwa wataendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuondoa au kupunguza ongezeko la watoto wa mitaani nchini huku akisema wataendelea kuibua vipaji vya watoto hao.

Hata hivyo waziri gwajima amesema kuwa wao kama wizara watasimamia kwa uadilifu na umakini wa hali ya juu katika kuhakikisha watoto hao wanaishi kama watoto wengine na kuibua vipaji vyao walivyonavyo ili watimize ndoto zao.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya huduma na maendeleo ya jamii Mh Stansilaus Nyongo amesema kuwa kituo hicho kitoe matokeo chanya katika malezi kwa kuwa bado kuna kundi kubwa la watoto wa mitaani na linahitaji msaada wa serikali katika malezi bora Huku akiomba wizara husika kuwaangalia watumishi wanao wahudumia watoto hao katika kituo hicho ili watoe huduma bora kwa watoto hao.

Naye mwakilishi wa shirika la ABBOTT FUND Natalia lobue  ambao wamefadhili ujenzi huo wa makao ya taifa ya kulelea watoto kikombo ameishukuru serikali ya Tanzania kwa kuendelea kutoa ushirikiano kwao katika kuhakikisha watoto wanao ishi mazingira magumu wanapata haki zao  za msingi.