Dodoma FM

Miradi ya TASAF yakosa ushirikishwaji baina ya mfuko, viongozi na jamii

7 December 2023, 9:47 pm

Njia ya ushirikishwaji katika utekelezaji miradi mbaimbali imekuwa  ikiongeza urahisi wa kuweka mikakati bora ya usimamizi.Picha na halmashauri ya Kigoma.

Aidha mabadiliko hayo ya malipo katika mfuko wa jamii wa kusaidia kaya maskini yalikuja yakiwa na lengo la kurahisisha utekelezi wa zoezi la utoaji fedha kwa walengwa.

Na Victor Chigwada.                                     

Imeelezwa kuwa kukosekana kwa nguvu ya ushirikishwaji katika miradi ya TASAF imekuwa chanzo cha kudumaza maendeleo baina ya mfuko,jamii pamoja na viongozi wa eneo husika

Anjero Lucasi Diwani wa Kata ya Mlowa barabarani adhaifu huo upo ndani ya baadhi ya vijiji vyake ambavyo vimekuwa vikitekeleza miradi iliyopo chini ya TASAF huku yeye kama kiongozi wa Kata asifahamu chochote

Amesema kuwa changamoto hiyo inaleta ugumu pale ambapo wananchi wanahitaji kusikia sauti ya kiongozi wa Kata iwatetee ile hali hukuna ushirikishwaji  uliofanyika mwanzoni

Sauti ya Anjero Lucasi Diwani wa Kata ya Mlowa barabarani .

Lucasi ameongeza nje na utekelezwaji wa miradi hiyo bila ushirikishwajii bado mabadiliko ya mfuko huo wa TASAF kutoka kwenye mlipo ya mkononi hadi malipo kwa njia ya simu

umekuwa changamototo miongoni mwa walengwa kutokana na kukosa watu sahihi wa kuwasimamia katika utoaji na upokeaji wa fedha hizo

Sauti ya Anjero Lucasi Diwani wa Kata ya Mlowa barabarani .

Aidha Lucasi amesema kuwa ni afadhali ya mfumo uliokuwa hapo mwanzo tofauti na mfumo wa sasa ambao jamii ya walengwa imekuwa ikiupigia kelele mfumo huo

Sauti ya Anjero Lucasi Diwani wa Kata ya Mlowa barabarani .