Dodoma FM

Barcelona hali tete kiuchumi

4 December 2020, 8:07 am

Barcelona,

Hispania.

Rais wa mpito wa klabu ya Barcelona Carlos Tusquets ameonya kuwa hali ya kifedha kwa sasa ni mbaya na inatia wasiwasi.

Kiongozi huyo aliyechukua mahala pa Josep Maria Bartomeu aliyejiuzulu mwezi Oktoba amesema klabu inapaswa ingekuwa imemuuza Messi.

Amesema wachezaji hawatapata mishahara yao ya Januari kutokana na hali ilivyo kwa sasa.

“Tutalazimika kutolipa wachezaji mishahara yao ya mwezi Januari hapo mwakani kutokana na hali ya kiuchumi ilivyo kwa sasa” ,amesemaTuesquests