Dodoma FM

Uchafuzi wa mazingira wachagiza mabadiliko ya hali ya hewa

30 May 2022, 5:01 pm

Na ;Victor Chigwada.

Matokeo ya mabadiliko ya Hali ya hewa nchini na hata dunia kwa ujumla yamekuwa yakichangiwa na shughuli za  uchafunzi wa mazingira ikiwa ni pamoja ukataji wa misitu ovyo

Suala la matumizi ya mikaa nchini limekuwa chachu ya kupelekea wananchi kuendelea na ukataji miti kwaajili ya kuzalisha mkaa hali inayopekea kuathili mazingira

Mwenyekiti wa Kijiji Cha Minguwi Kata ya Pwaga Wilaya ya Mpwapwa Bw.George Mkombola amekiri sula hili linatokana na ukosefu wa elimu ya mazingira pamoja na ukaidi kwa baadhi ya watu.

Aidha Diwani wa Kata hiyo Bw.Wilisoni Mgonela amesema kuwa kiburi Cha changamoto hiyo kinatokana na sheria kukosa uzito kwani watuhumiwa wanalipa faini na kurudi mtaani Hali inayowakatisha tamaa wale wanaofuata na kutimiza wajibu wa Sheria

.

Suala hili la faini ya ukataji miti kimekuwa likilalamikiwa maeneo mengi kwani watu wamekuwa wakiharibu mazingira kwa kutokuogopa faini ya hilingi laki tatu hivyo Ni vema Serikali kupitia na kufanya mabadiliko katika Sheria hii