Dodoma FM

Machinga Dodoma wampongeza Rais Samia

23 March 2023, 5:36 pm

Wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama machinga wakiwa katika mkutano wa kumpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu. Picha na Thadei Tesha.

Ni mkutano uliowakutanisha wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama machinga ambapo awali ulitanguliwa na maandamano ya amani kwa ajili ya kumshukuru Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kutimiza miaka miwili madarakani.

Na Thadei Tesha.

Wafanyabiashara wa biashara ndogondogo maarufu kama machinga jijini Dodoma wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh Samia Suluh kwa kuwajengea mazingira rafiki ya kufanyia biashara zao.

Akizungumza katika mkutano huo Mwenyekiti msaidizi wa machinga mkoa wa Dodoma bw Christian msumari anatumia fursa hii kueleza yale aliyoyafanya rais kwa ajili ya kulisaidia kundi la wamachinga.

Wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama machinga wakiimba wimbo wa Taifa katika mkutano huo wa kumpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu. Picha na Thadei Tesha.

Viongozi wengine walioshiriki katika hafla hiyo maalum ni pamoja na Mh. Davis Mwamfupe Mstahiki Meya wa jiji la Dodoma, Abeid msangi ambaye ni Afisa biashara wa Jiji la Dodoma aliyemwakilisha Mkurugenzi wa jiji pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mh. Jabir Shekimweri ambapo kwa pamoja wamemshukuru Rais wa Tanzania kwa kuendelea kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya machinga kufanya biashra.

Sauti za viongozi

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rosemary Senyemule ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo amesema soko la machinga ni miongoni mwa masoko ya mfano ambapo kujengwa kwa soko hilo kunatokana na juhudi za viongozi mbalimbali akiwemo Rais Samia Suluh Hasan.

Sauti ya Mh.Rosemary Senyemule ni mkuu wa Mkoa wa Dodoma