Dodoma FM

Jamii yahimizwa kutumia maziwa kwa wingi kujenga afya

21 June 2023, 4:54 pm

Kaimu muuguzi mfawidhi wa hosptali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma akizungumza wakati akipokea maziwa kutoka Bodi ya maziwa kwaajili ya wagonjwa.Picha na Mariam Matundu.

katika kuadhimisha wiki ya utumishi wa umma bodi ya maziwa imefika katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kutoa elimu ya umuhimu wa kutumia maziwa salama pamoja na kugawa maziwa katika baadhi ya wodi za wagonjwa hospitalini hapo.

Na Mariam Matundu.

Tabia ya unywaji maziwa kwa jamii bado hairidhishi hapa nchini kutokana na takwimu za bodi ya maziwa kuonesha wastani wa unywaji wa maziwa kuwa lita 47 kwa kila mtu kwa mwaka, huku shirika la chakula duniani FAO likipendekeza unywaji wa lita 200 kwa kila mtu kwa mwaka .

kufuatia hali hii wadau mbalimbali wanaendelea kutoa elimu ya unywaji wa maziwa salama kwa watu wote kutokana na umuhimu wake kwenye mwili wa binadamu.

Patricia Kabendela ni kaimu muuguzi mfawidhi wa hosptali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma wakati akipokea maziwa kutoka bodi ya maziwa kwa ajili ya wagonjwa ameeleza umuhimu wa maziwa katika kujenga afya .

Sauti ya muuguzi mfawidhi……
Baadhi ya wafanyakazi kutoka Bodi ya Maziwa wakikabidhi maziwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma. Picha na Mariam Matundu,

Aidha ameishukuru bodi ya maziwa kwa kupeleka maziwa kwa ajili ya wagonjwa na kuwaomba wadau wengine kujitokeza kupeleka maziwa hospitalini hapo .

Sauti ya muuguzi mfawidhi…………

Nae Neema Moshi mteknolojia wa chakula kutoka bodi ya maziwa amesisitiza juu ya matumizi ya maziwa yaliyo salama .

Sauti ya mteknolojia wa chakula .
Wadau wengine wanaombwa kuendelea kupeleka maziwa kwaajili ya wagonjwa . Picha Mariam Matundu.

Baadhi ya wagonjwa walipatiwa maziwa ameshukuru bodi ya maziwa kwa kuwapelekea maziwa pamoja na elimu ya umuhimu wa maziwa .

Sauti za Baadhi ya wagonjwa.