Dodoma FM

Wakazi wa Chaduru waomba serikali ikamilishe soko la Tambukareli

23 May 2023, 6:30 pm

Muonekano wa soko hilo ambalo kwa sasa halitumiki na wafanyabiashara. Picha na Thadei Tesha.

Miundombinu ya soko hilo inaelezwa  kuwa mibovu na kusababisha wafanyabiashara kushindwa kufanya biashara ndani ya eneo hili.

Na Thadei Tesha.

Baadhi ya wananchi wa kata ya Chaduru jijini Dodoma wameiomba serikali kukamilisha kwa haraka miundombinu ya soko la Tambukareli ili waweze kuanza kufanya biashara kwa haraka.

Dodoma Tv imewatembelea na kufanya mahojiano na baadhi ya wafanyabiashara na wakazi wa eneo hilo ambapo wanasema kuwa soko hilo limekuwa katika mazingira ambayo si rafiki kwa muda mrefu jambo linalopelekea wafanyabiashara kushindwa kufanya biashara.

Sauti za baadhi ya wakazi wa kata ya Chaduru.
Wakazi wa eneo hilo la karibu na soko hilo la Tambukareli wakizungumza na Dodoma Tv. Picha na Thadei Tesha.

Aidha Dodoma Tv imemtafuta Mwenyekiti wa soko la Tambukareli jijini hapa naye akawa na haya ya kuzungumza.

Sauti ya Mwenyekiti wa soko.