Dodoma FM

Taka ngumu zatajwa kuharibu mifumo ya maji taka

20 March 2023, 3:25 pm

Mkurungenzi wa Huduma za usambazaji maji na usafi wa mazingira Duwasa Mhandisi Emmanuel Mwakabole. Picha na Mariam Kasawa.

Jiji la Dodoma linakisiwa kuzalisha tani 350 za taka ngumu kwa siku ambapo kata za nje ya mji uzalishaji tani 114 na Kata za mjini uzalisha ni tani 236.

Na Mindi Joseph.

Utupaji wa taka Ngumu Ovyo umetajwa kuwa na athari kubwa katika Mifumo  ya maji taka.

Akizungumza na Taswira ya habari Mkurungenzi wa Huduma za usambazaji maji na usafi wa mazingira Duwasa Mhandisi Emmanuel Mwakabole amesema ni marufuku kutupa taka ovyo huku akiutaja mtaa wa Madukani kuongoza katika kutupa taka.

Amesema wanashirikiana na jiji la dodoma  ili kuwachukulia hatua wale wanaobainika kutupa taka ngumu ovyo.

Sauti ya Mhandisi Emmanuel Mwakabole