Dodoma FM

Watendaji wa serikali watakiwa kutatua kero za wananchi

25 October 2023, 1:02 pm

Picha ni wakazi wa eneo la Mwanachugu Bahi sokoni wakiwa katika Mkutano huo. Picha na Bernad Magawa.

Katika Mkutano huo Mkuu wa wilaya ya Bahi Mh Godwin Gondwe aliambatana na kamati ya usalama ya wilaya hiyo.

Na Bernad Magawa

Mkuu wa wilaya ya Bahi Mheshimiwa Godwin Gondwa amewaagiza watendaji wa Serikali  katika ngazi zote wilayani humo kuhakikisha wanasikiliza na kutatua kero zao kikamilifu huku akisema kuwa hatua kali za kiutumishi zitachukuliwa kwa wale  watakaoshindwa kutekeleza agizo hilo.

Mheshimiwa Gondwe ameyasema hayo kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Bahi Sokoni  eneo la Mwanachugu kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi huku akiambatana na kamati ya usalama ya wilaya hiyo, wakuu wa Idara pamoja na wakuu wa taasisi za serikali  na kuongeza kuwa  wilaya imetenga siku ya Alhamisi kuwa  siku maalumu ya kusikiliza kero za wananchi.

Sauti ya Mh. Godwin Gondwe.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Bahi Zaina Mlawa amewaagiza viongonzi wa serikali za vijiji kuhakikisha wanasoma mapato na matumizi kwenye mikutano ya hadhara huku akiwasihi wananchi kuendelea kuwatumia vongozi wao katika kusikiliza na kutatua kero zinazowakabili.

Sauti ya Bi. Zainab Mlawa.

Awali, Wananchi waliokusanyika katika mkutano huo walipata nafasi ya kueleza kero mbalimbali zinazowakabili  ambapo pamoja na mambo mengine bado suala la kukosekana kwa soko wilayani hapo likiendelea kuwa kero kwa wafanyabiashara na kusema kuwa linaongeza ugumu wa maisha kwa wananchi wa Bahi.

Sauti za wananchi