Dodoma FM

Kukatika kwa Umeme kunaathiri upatikanaji wa maji Kongwa

10 April 2023, 12:53 pm

Maji yakiwa yanatoka katika moja ya mabomba wilayani Kongwa. Picha na Mindi Joseph.

Duwasa imeendelea kuhimiza utunzaji wa miundombinu ya maji safi iliyopo katika maeneo yao ili iweze kudumu kwa muda mrefu.

Na Miandi Joseph.

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira  Dodoma (DUWASA) imesema kukatika mara kwa mara kwa huduka ya umeme kunaathiri uzalishaji na usambazaji wa maji katika maeneo ya kongwa na kibaigwa.

Mkurugenzi wa huduma za usambazaji maji na usafi wa mazingira DUWASA Eng Emmanuel Mwakabole amesema  kongwa na kibaigwa ni miongoni mwa maeneo ambayo yanaathirika zaidi na makatizo ya umeme.

Sauti ya Mkurugenzi wa huduma za usambazaji maji na usafi wa mazingira DUWASA

Amesema Maeneo hayo yamekuwa yakiathirika na upatikanaji wa majisafi kufuatia kusuasua kwa huduma ya umeme ambayo mara zote imeelezwa na  Tanesco ni ubadilishaji wa nguzo katika njia mbalimbali zenye uhusiano na usukumaji wa maji.

Mkurugenzi wa huduma za usambazaji maji na usafi wa mazingira DUWASA