Dodoma FM

Malipo yakwamisha urasimishaji wa ardhi Ihumwa

6 March 2024, 6:54 pm

Wananchi wamekuwa hawana hamasa ya kulipia viwanja vyao ambavyo tayari vimesha pimwa.Picha na google.

Zoezi hilo la urasimishaji linahusisha zaidi ya viwanja 2500 kwa upande wa mtaa wa ihumwa A ambapo inaelezwa kwa ni viwanja visivyozidi 100 ndivyo vimelipiwa.

Na Victor Chigwada.
Kusuasua kwa Malipo ya zoezi la Urasimishaji wa ardhi katika kata ya Ihumwa imetajwa kukwamisha zoezi hilo .
Akizungumza na Taswira ya Habari mwenyekiti wa kamati ya urasimishaji ardhi Ihumwa Bw.Mathayo Ulalo ambaye amekiri zoezi la urasimishaji kwa sasa limesimama kutokana na kusubiri fedha za kuendesha zoezi hilo.
Amesema kuwa kupitia bajeti mpya wanayo isubiri wanatarajia kuyafikia maeneo ambayo bado hayajapimwa ikiwa ni sambamba na uchongaji wa barabara za mitaa.

Sauti ya Bw.Mathayo Ulalo .

Ulalo ameongeza kuwa wananchi wamekuwa hawana hamasa ya kulipia viwanja vyao ambavyo tayari vimesha pimwa ili waweze kupata hati miliki za viwanja hivyo
Aidha ametoa wito kwa wananchi kuchangamkia fursa hiyo ya kulipia viwanja ambavyo tayari vimeshapimwa .

Sauti ya Bw.Mathayo Ulalo .

Nao baadhi ya wananchi wameishukuru Serikali kwakuja na wazo la urasimishaji kwani utasaidia kuondoa migogoro ya mipaka .

Sauti za wananchi.