Dodoma FM

Wazazi wametakiwa kuwapataia watoto muda wa kujisomea

23 July 2021, 12:26 pm

Na ; Benard Filbert.

Wazazi wametakiwa kuwapunguzia majukumu ya kifamilia watoto wao ambao wapo madarasa ya mitihani ili waweze kujisomea.

Hayo yameelezwa na diwani wa kata ya Chemba bw. Gadri Lukumai wakati akizungumza na taswira ya habari ambapo amesema kuwa kufuatia baadhi ya wazazi kuwapa majukumu mazito wanafunzi ambao wapo madarasa ya mitihani wameamua wanafunzi hao wakae kwenye kambi ili waweze kujisomea zaidi.

Amesema endapo watoto hao watakaa kwenye kambi katika shule zao watakuwa na muda mwingi wakusoma kuliko kufanya vitu vingine.

Kadhalika ameongeza kuwa elimu ndio ufunguo wa maisha hivyo kila mzazi anatakiwa kutekeleza wajibu huo.

Hivi karibuni mkuu wa mkoa wa Dodoma Bw. Antony Mtaka alitoa maagizo kwa wazazi na viongozi mbalimbali kuhakikisha wanawapunguzia majukumu katika familia wanafunzi ambao wapo katika madarasa ya mitihani ili kuepuka kuathiri masomo yao hususani kuelekea kipindi cha mitihani.

Wanafunzi ambao wapo katika madarasa ya mitihani wanatakiwa kupewa muda wakutosha ili kujiandaa na mitihani yao kuepuka kufanya vibaya.