wananchi wa Igunguli
Dodoma FM

Igunguli waomba msaada ujenzi wa Zahanati

30 January 2023, 9:28 am

Na; Victor Chigwada.

Ujenzi wa zahanati Igunguli.

Wananchi wa kijiji cha Igunguli Kata ya Loje Wilaya ya Chamwino wameiomba Serikali kuwaunga mkono  na kuwasaidia kukamilisha ujenzi wa zahanati

Wakizungumza na taswira ya habari wamesema  kukosekana kwa huduma ya afya kijiji hapo inasababisha wananchi kwenda kutafuta huduma ya afya kwenye Vijiji vya Jirani

Wananchi sauti.

Mwenyekiti wa kijiji cha Igunguli Bw.Hamisi Msangi amesema kuwa hatua wanayoifanya kwa sasa  ni Ujenzi wa zahanati   ili kupunguza adha ya umbali mrefu na kukosekana kwa zahanati kijijini hapo

Mwenyekiti sauti.

Msangi amesema ushiriki wa wananchi kupitia Nguvu kazi  haitoshi tu kukamilisha ujenzi huo kutokana na gharama za maisha kubadilika .

Sauti mwenyekiti.

Naye Diwani wa Kata ya Loje Bw.John Njohoka amesema zahanati iliyopo kwa sasa imelemewa na wagonjwa hali ambayo wamewasilisha maombi ya ujenzi wa kituo cha afya