Dodoma FM

Wafanyabiashara Sabasaba walia na ugumu wa biashara

16 March 2023, 8:36 am

Muonekano wa eneo la Sabasaba kwa sasa ambapo hapo awali ilikuwa stendi ya Daladala. Picha na Thadei Tesha.

Awali daldala za jiji la dodoma zilikuwa na kituo kikuu katika soko la sabasaba kabla ya kuhamishiwa kituo katika soko jipya la machinga complex.

Na Thadei Tesha.

Zikiwa zimepita wiki chache tangu kuhamishwa kwa daldala katika eneo la sabsaba jijini dodoma wafanyabiashara katika eneo hilo wamesema hali ya biashara imezidi kuwa ngumu katika eneo hilo.

Dodoma tv imefika katika soko la sabasaba na ambapo zilikuwepo daladala na kukuta hali hii baadhi ya wafanyabiashara wanasema hali ya biashara kwa sasa ni ngumu kwani hakuna wateja kama ilivyokuwa hapo awali.

Sauti za wafanya biashara.

Aidha baadhi ya wafanyabiashara hao wameiomba serikali kuweka angalau kituo ndani ya soko hilo au kubuni utaratibu utakoaziruhusu daladala kupita ili waweze kunufaika pande zote mbili kati ya soko la machinga na soko la sabsaba.

Sauti za Wafanya biashara.