Dodoma FM

Madereva bodaboda wanaoendekeza tamaa Bahi waonywa

25 October 2023, 1:25 pm

Picha ni baadhi ya Madereva bodaboda kati ya moja ya vijiwe wilayani Bahi. Picha na Bernadi Magawa.

Bodaboda wamekuwa na mazoea ya kukodiwa usiku wa manane na watu ambao hawawafahamu matokeo yake wanauawa na kuporwa pikipiki.

Na. Bernad Magawa.

Kamanda wa Polisi wilaya ya Bahi SSP Idd Ibrahim amekemea vikali madereva wa bodaboda wanaoendekeza tamaa ya fedha kwa kukodiwa na watu wasiowafahamu kwa ahadi ya kulipwa ujira mkubwa huku akiwakumbusha wananchi kuacha kuhifadhi wageni wasiowafahamu bila kutoa taarifa kwa viongozi wa serikali.

Akizungumza na wananchi kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Bahi sokoni SSP Idd Ibrahim amesema bodaboda wamekuwa wakijali fedha kuliko  uhai wao jambo ambalo  ni hatari.

Sauti ya SSP Idd Ibrahim.
Bodaboda wamekuwa wakijali fedha kuliko  uhai wao jambo ambalo  ni hatari.Picha na Bernad Magawa.

Aidha amesema bodaboda wamekuwa na mazoea ya kukodiwa usiku wa manane na watu ambao hawawafahamu matokeo yake wanauawa na kuporwa pikipiki huku akieleza mbinu wanazopaswa kuzitumia kabla ya kuamua kukodiwa hasa nyakati za usiku.

Sauti ya SSP Idd Ibrahim.

SSP Idd Ibrahim pia amewaeleza wananchi madhara ya kuwapa hifadhi wageni  wasiowafahamu huku akikemea vikali watu wanaonunua simu janja zilizotumika na kusema kuwa kwa sasa ni hatari na wanaweza kufungwa kupitia simu hizo bila hatia.