Dodoma FM

Ujenzi wa madarasa wasaidia kupunguza mrudikano wa wanafunzi chemba

19 January 2022, 2:30 pm

Na ;Benard Filbert.

Ujenzi wa madarasa mapya yaliyojengwa kwa fedha za uviko 19 katika kata ya chemba wilayani Chemba imesaidia kupunguza mrundikano wa wanafunzi katika shule ya sekondari Chemba

Hayo yameelezwa na diwani wa kata ya Chemba bwana Gadiel Lukumai wakati akizungumza na taswira ya habari kuhusu hali ya wanafunzi mara baada ya kufunguliwa kwa shule zote nchini.

Amesema kufuatia kujengwa kwa madarasa mapya katika shule ya sekondari ya Chemba imesaidia kupunguza mlundikano wa wanafunzi madarasani.

Hata hivyo ameongeza kuwa hivi sasa hamasa imekuwa kubwa kwa wazazi kupeleka watoto shuleni ambapo hivi sasa wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari walioripoti shuleni ni wengi.

Hata hivyo amewataka wazazi kuhakikisha wanawapeleka watoto shuleni kwani hivi sasa hakuna kisingizio cha uhaba wa madarasa.