Dodoma FM

Viongozi watakiwa kuzingatia sheria za maadili ya umma

4 January 2024, 5:09 pm

Picha ni Bi. Lidya Mwakibete Afisa Maadili ya viongozi wa umma akiongea na Dodoma Tv.Picha na Aisha Alim.

Hayo yamesemwa na Alfred Mboya Afisa maadili kutoka secretariete ya maadili ya viongozi wa umma wakati akifanya mahojiano na Dodoma Tv.

Na Aisha Alim.
Viongozi wa umma wametakiwa kuzingatia sheria za maadili ya viongozi katika Taasisi zao ili wawe mfano wakuigwa ndani ya jamii

Amewataka viongozi kufuata sheria na kanuni katika kufanya maamuzi ili kuzingatia sheria ya viongozi wa umma.

Sauti ya Bw. Alfred Mboya
Picha ni Mkazi wa Jijini Dodoma akitoa maoni yake kuhusu viongozi. Picha na Aisha Alim.

Kwa upande wake Bi. Lidya Mwakibete afisa maadili ya viongozi wa umma amesisitiza suala la usawa kwa viongozi bila kufanya ubaguzi wakati wa kutekeleza majukumu yao

Sauti ya Bi. Lidya Mwakibete.

Wananchi waliozungumza na kituo hiki juu ya wajibu wa watumishi wa umma kuonesha sifa njema wamesema matarajio ya yao ni kuona kiongozi bora akileta usawa kwa jamii pamoja na kuwajibika na hatimae kuleta maendeleo.

Sauti za Wananchi.