RUWASA manyara kufanya tathmini ya upatikanaji wa maji katika Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima
5 August 2026, 17:04

Na Hamis Kitana.
Katika ziara hiyo, Waziri Aweso ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwekeza katika sekta ya elimu na kuhakikisha Watanzania wa makundi yote wanapata fursa ya kujifunza na kujipatia ujuzi utakaowasaidia kuboresha maisha yao.
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, ameiagiza RUWASA Mkoa wa Manyara kufanya tathmini ya upatikanaji wa maji katika Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima iliyopo Mtaa wa Miomboni, mjini Babati, na kuchimba kisima kitakachohakikisha taasisi hiyo inapata huduma ya maji safi na salama kwa uhakika.
Aweso ametoa maelekezo hayo wakati wa ziara maalumu ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali, baada ya kupokea taarifa kuhusu changamoto ya upatikanaji wa maji inayolikabili kituo hicho kinachotoa mafunzo ya fani mbalimbali kwa watu waliokosa fursa ya kuendelea na elimu ya msingi au sekondari.