Dodoma FM

Changamoto ya umeme kutatuliwa mgodi wa Manyemba

23 September 2026, 17:08

Pich ni zoezi la usambazaji wa umeme katika maeneo mbalimbali ya nchi mjini na vijjini. Picha na mwananchi.

Hatua za kutatua changamoto ya ukosefu wa umeme katika Mgodi wa Manyemba, Kata ya Dabalo, Wilaya ya Chamwino, zimeanza kuchukuliwa baada ya wachimbaji na wawekezaji kukosa nishati hiyo kwa muda mrefu, huku TANESCO Wilaya ya Chamwino ikiahidi kufikisha umeme katika mgodi huo.

Na Victor Chigwada.

Hatua za kutatua changamoto ya ukosefu wa nishati ya umeme katika Mgodi wa Manyemba, Kata ya Dabalo, Wilaya ya Chamwino, zimeanza kuchukuliwa baada ya wachimbaji na wawekezaji katika mgodi huo kukosa umeme kwa muda mrefu.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Maendeleo wa Kata ya Dabalo, Omary Kiguna, ambaye amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kusema kuwa TANESCO Wilaya ya Chamwino imeahidi kufikisha umeme katika mgodi huo muda wowote.

Simulizi na Victor Chigwada.

Baadhi ya wachimbaji katika mgodi huo wamesema kero kubwa inayowakabili ni ukosefu wa nishati ya umeme, hali inayowalazimu kutumia mafuta ya dizeli ambayo yamekuwa yakiongeza gharama za uzalishaji.

Simulizi na Victor Chigwada.