Wananchi chamwino wataja matarajio kwa mbunge mpya
4 November 2026, 16:33

Wananchi wa Chamwino sasa wanaelekeza macho yao kwa mwakilishi watakayempata, wakisubiri kuona namna atakavyogeuza imani waliyoitoa kupitia kura kuwa matokeo yanayoonekana katika maendeleo ya jimbo hilo.
Na Anwary Shabani.
Ushiriki wa wananchi katika uchaguzi hauishii kwenye kupiga kura pekee, bali pia unabeba matumaini na matarajio ya kupata uongozi utakaosimamia maendeleo yao. Hayo yamebainika kwa baadhi ya wananchi wa Jimbo la Chamwino jijini Dodoma baada ya kushiriki zoezi la upigaji kura, wakieleza matarajio yao kwa mbunge wa jimbo hilo.

Wananchi hao wamesema wanatarajia kupata mwakilishi atakayekuwa karibu nao, kusikiliza kero zao na kuzifanyia kazi, hususan katika sekta za elimu, afya, miundombinu na huduma nyingine za kijamii.