Dodoma FM

Ajinyonga siku moja kabla ya harusi ya mwanae

19 October 2026, 16:14

Picha ni gari ya Polisi ikiwa katika eneo la tukio kijijini hapo.Picha na Kitana Hamis.

Tukio hilo limetokea wakati familia ya marehemu ikiwa katika maandalizi ya mwisho ya harusi ya mtoto wake wa mwisho wa kiume, ambaye alitarajia kufunga ndoa, Oktoba 17, 2026.

Na Kitana Hamis.

Mwanamke mmoja alie fahamika kwa jina la Mwanaisha Saidi Juma, mwenye umri wa miaka 70, mkazi wa Kitongoji cha Madibira, Kata ya Magugu, Wilaya ya Babati, Mkoa wa Manyara, amefariki dunia baada ya kudaiwa kujinyonga usiku wa kuamkia Oktoba 16, 2026 huku Chanzo cha tukio hilo kikiwa bado hakijafahamika.

Tukio hilo limetokea wakati familia ya marehemu ikiwa katika maandalizi ya mwisho ya harusi ya mtoto wake wa mwisho wa kiume, ambaye alitarajia kufunga ndoa, Oktoba 17, 2026.

Akizumgumzia tukio hilo, mtoto wa marehemu, Sadik Musa, amesema kuwa hakukuwa na changamoto yoyote katika maandalizi ya harusi hiyo ambayo ingeweza kumsababishia mama yake msongo wa mawazo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Madibira, Omary Rajab, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, huku Jeshi la Polisi limefika eneo la tukio na kufanya uchunguzi wa mwili wa marehemu ambapo umebaini kuwa kifo hicho kimetokana na kujinyonga na kukosa hewa ya kupumua.

Ripoti ya Kitana Hamis.