Dodoma FM

Wafanyabiashara wahimizwa kulipa kodi kwa maendeleo ya taifa

24 November 2026, 16:56

Picha ni mfanya biashara akiwa na mtoa huduma kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania. Picha na BMG Digital.

Wafanyabiashara wanahimizwa kuzingatia wajibu wao wa kulipa kodi kwa wakati na kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa, kwani hatua hiyo ni sehemu muhimu ya kujenga uchumi imara, kuimarisha huduma za kijamii na kuchochea maendeleo endelevu ya taifa.

Na Mwanaidi Mpetu.

Wananchi wametakiwa kutambua umuhimu wa ulipaji kodi kwa wafanyabiashara, wakizingatia kuwa kodi ni chanzo muhimu cha mapato ya serikali yanayowezesha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na kuboresha huduma za kijamii.

Hata hivyo, pamoja na umuhimu wa ulipaji kodi, bado kuna haja ya kuendelea kutoa elimu kwa wafanyabiashara kuhusu wajibu wao wa kulipa kodi na faida zake katika kukuza uchumi wa nchi.

Baadhi ya wananchi wameeleza mitazamo yao kuhusu umuhimu wa wafanyabiashara kulipa kodi, wakibainisha namna mchango huo unavyosaidia kuongeza mapato ya serikali na kuchochea maendeleo ya taifa.

Sauti za wananchi.

Kwa upande wake, mchambuzi wa masuala ya uchumi, ambaye pia ni mhadhiri wa sayansi ya siasa katika chuo kikuu cha dodoma, bw. Hamis issa, anaeleza umuhimu wa wafanyabiashara kulipa kodi, akigusia mchango wake katika kukuza uchumi, kuongeza mapato ya serikali na kuboresha huduma za kijamii.

Sauti ya Mchambuzi wa masuala ya uchumi Bw. Hamis issa.