Mvua za El nino zisiwesababu ya wananchi kisitisha kilimo
8 October 2026, 14:07

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Rosemary Senyamule wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya mvua kubwa zinazotarajiwa kwa kufuatilia utabiri wa hali ya hewa na kuzingatia ushauri unaotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, TMA.Ziara hiyo imelenga kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo hayo, pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Na Anwary Shabani.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, amewataka wananchi wa Halmashauri ya Wilaya na Mji wa Kondoa kuendelea na shughuli za kilimo licha ya tahadhari ya mvua kubwa zinazotarajiwa, huku akisisitiza umuhimu wa kuzingatia utabiri na ushauri wa wataalamu ili kujilinda dhidi ya madhara yanayoweza kujitokeza.
Mhe. Senyamule ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa na Halmashauri ya Mji wa Kondoa, ambapo amekagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kusikiliza pamoja na kutatua kero mbalimbali za wananchi.
Hata hivyo, Mhe. Senyamule amesema tahadhari hiyo isiwe sababu ya wananchi kusimamisha shughuli za kilimo, bali watumie mvua zinazotarajiwa kama fursa ya kuongeza uzalishaji wa chakula, huku wakizingatia maelekezo ya wataalamu kuhusu maeneo salama na muda unaofaa kwa shughuli za kilimo.

Ameongeza kuwa wananchi wanapaswa kuchukua hatua za tahadhari bila kusimamisha shughuli za uzalishaji, ikiwemo kilimo, ili kuhakikisha mvua hizo zinakuwa fursa ya kuinua uzalishaji na kuboresha maisha ya wananchi.
Ziara hiyo imelenga kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo hayo, pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.