Dodoma FM

Wananchi watakiwa kutambua utarabu na sheria ya kumiliki silaha

23 November 2026, 17:43

Uzingatiaji wa sheria zinazohusu umiliki wa silaha pamoja na matumizi sahihi ni muhimu katika kulinda usalama wa watu.Pichana BBC.

Uzingatiaji wa sheria zinazohusu umiliki wa silaha pamoja na matumizi sahihi ni muhimu katika kulinda usalama wa watu, kuzuia matumizi mabaya ya silaha na kuhakikisha uwajibikaji kwa wanaomiliki silaha kisheria.

Na Mwanaidi Mpetu.

Imeelezwa kuwa umiliki wa silaha unahitaji kufuata taratibu za kisheria zilizowekwa na mamlaka husika ili kuhakikisha usalama wa mmiliki na jamii kwa ujumla.

Wakizungumza kuhusu utaratibu wa umiliki wa silaha kisheria pamoja na matumizi sahihi ya silaha hizo, baadhi ya wananchi wamesema hawana uelewa wa kutosha kuhusu suala hilo .

Sauti za wananchi.

Mabenga Gitui ni Mwanasheria kutoka chuo cha mtakatifu Agostino yeye anaeleza kuwa umiliki wa silaha kisheria unapaswa kuzingatia taratibu, masharti na vibali vinavyotolewa na mamlaka husika, huku akifafanua wajibu wa mmiliki wa silaha na sheria zinazopaswa kuzingatiwa katika matumizi yake.

Sauti ya Mabenga Gitui.