Dodoma FM
9 November 2026, 17:12

Mazungumzo ya wazi yamekuwa hatua ya kwanza kabla ya kufika kituo cha afya kupata ushauri wa kitaalamu.
Na Bennedict Ngelangela.
Kwa muda mrefu mjadala wa matumizi ya uzazi wa mpango umeonekana kuwa wa wanawake pekee. Kliniki nyingi za afya ya uzazi hujaa wanawake huku wanaume wakibaki pembeni, kana kwamba suala hilo halihusiani nao.
Hata hivyo, uzoefu wa baadhi ya wanaume unaonyesha kuwa ushiriki wao unaweza kubadilisha kabisa ustawi wa familia kuanzia afya ya mama hadi hali ya kiuchumi ya nyumbani.
Katika familia nyingi, maamuzi ya uzazi wa mpango yanaweza kuibua mijadala mikali au hata migogoro.