Dodoma FM
9 November 2026, 16:37

Lugha ya alama imeendelea kuwa nyenzo muhimu katika kurahisisha mawasiliano kati ya watu wenye uziwi na jamii inayowazunguka, lakini zaidi ya mawasiliano, lugha hiyo inaweza kuwa daraja la kuwafungulia fursa mbalimbali za kiuchumi, ajira na maendeleo.
Hata hivyo, bado kuna uhitaji wa jamii kutambua umuhimu wa kujifunza lugha hiyo ili kuongeza ushiriki wa watu wenye uziwi katika shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi.
Mwandishi wetu Anwary Shabani amefanya mahojiano na Amani Matiasi ambaye ni mkalimani wa lugha za alama kwa viziwi nae anaetuleza zaidi kuhusu umuhimu wa lugha za alama na kama fursa kwa vijana wa ki Tanzania.