Wakazi wa Mlowa waomba msaada ujenzi wa mabweni
29 September 2026, 17:09

Tayari mpango wa ujenzi wa mabweni shuleni hapo umeanza kufanyiwa kazi.
Na Victor Chigwada.
Wakazi wa Mlowa barabarani Wilayani Chamwino wameiomba Serikali na wadau mbalimbali kuwasaidia kujenga mabweni katika shule ya sekondari yao ili kusaidia watoto wanao toka mbali pamoja na kuongeza ufaulu.
Wamesema kupitia fursa ya kukaa shuleni itasaidia kupata muda mwingi wa kujisomea Kwa utulivu sambamba na kuondokana na vishawishi vya mtaani vinavyo weza kupelekea kukatisha masomo yao .
Naye Diwani wa Kata hiyo Anjero Lukas amesema tayari mpango wa ujenzi wa mabweni shuleni hapo umeanza kufanyiwa kazi hivyo wazazi wawe wavumilivu pia shule hiyo ina mpango wa kuongeza vyumba vya madarasa kwaajili ya kidato cha tano na sita.