Dodoma FM

Umuhimu wa tafiti za kisayansi wasisitizwa kutatua changamoto za jamii

30 October 2026, 16:45

Picha ni mtaalamu wa wa masuala ya utafiti akifanya uchunguzi wa kisayansi. Picha na Baraza la kisayansia kitaifa.

Matumizi ya ushahidi wa kisayansi badala ya kutegemea mazoea na dhana zisizothibitishwa yametajwa kuwa njia muhimu ya kupata suluhisho sahihi kwa changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii, huku tafiti na bunifu zikihimizwa kuwa sehemu ya maisha ya kila siku.

Na Daniel Njau.

Kukosekana kwa matumizi sahihi ya tafiti na bunifu za kisayansi kunaweza kuchelewesha upatikanaji wa suluhisho la changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii, hali inayodhihirisha umuhimu wa kizazi cha sasa kujenga utamaduni wa kufanya tafiti na kutumia matokeo yake kuboresha maisha ya kila siku.

Daktari Issa Mshani, mtafiti wa magonjwa ya kuambukiza na mifumo ya kiteknolojia katika afya ya jamii kutoka Taasisi ya Afya ya Ifakara, amesema tafiti zina mchango mkubwa katika kubaini chanzo cha changamoto na kupata suluhisho lake kwa kuzingatia ushahidi unaopatikana kupitia uchunguzi wa kisayansi.

Kwa upande wao, baadhi ya wananchi, wakiwemo vijana, wamesema maendeleo ya teknolojia yameongeza matumizi ya akili mnemba katika kufanya tafiti zinazohusu afya, mazingira, magonjwa na mimea, lakini matumizi yasiyo sahihi ya teknolojia hiyo yanaweza kusababisha matokeo yasiyoaminika.

Daktari Mshani amesisitiza umuhimu wa wazazi na jamii kuwaandaa watoto na vijana kupenda kufanya tafiti na kukuza ubunifu tangu wakiwa wadogo, akieleza kuwa ushiriki wa jamii ni muhimu katika kuibua na kutatua changamoto zinazohitaji uchunguzi na uvumbuzi wa kisayansi.

Simulizi na Daniel Njau.