Dodoma FM

Wananchi watakiwa kuto fumbia macho matukio ya uhalifu

9 November 2026, 16:51

Wananchi wana nafasi kubwa katika kupambana na vitendo hivyo kwa kushirikiana na vyombo vya usalama.Picha na Dodoma fm.

Hata hivyo, mapambano dhidi ya uhalifu yanahitaji ushiriki wa kila mwanajamii kwa kuwa usalama ni jukumu la pamoja na msingi muhimu wa amani na maendeleo ya jamii.

Na Mwanaidi Mpetu

Uhalifu ni miongoni mwa changamoto zinazoendelea kuikabili jamii katika maeneo mbalimbali, hali inayosababisha hofu, ukosefu wa usalama pamoja na kuathiri maendeleo ya wananchi.

Hata hivyo, wananchi wana nafasi kubwa katika kupambana na vitendo hivyo kwa kushirikiana na vyombo vya usalama na kutoa taarifa za uhalifu unaojitokeza katika maeneo yao.

Baadhi ya wananchi wanasema wamekuwa wakichukua hatua mbalimbali katika kukabiliana na uhalifu, ikiwemo kuanzisha ulinzi shirikishi, kutoa taarifa kwa vyombo vya dola pamoja na kuimarisha mshikamano baina ya wakazi wa maeneo husika.

Sauti za wananchi.

Mrakibu msaidizi wa jeshi la polisi na mkuu wa polisi jamii wilaya ya kipolisi Mtumba jijini Dodoma Charles Mwamtobe anasema kuwa mapambano dhidi ya uhalifu yanahitaji ushirikiano wa karibu kati ya wananchi na vyombo vya dola, huku akisisitiza umuhimu wa wananchi kutoa taarifa kwa wakati na kuepuka kujichukulia sheria mkononi.

Sauti ya Inspecta Charles Mwamtobe.

Aidha, wananchi wanahimizwa kujenga utamaduni wa kuripoti vitendo vya uhalifu, kuelimishana kuhusu masuala ya usalama na kushirikiana katika kutambua viashiria vya uhalifu kabla havijaleta madhara makubwa.