Usafi wa mazingira watambuliwa kama kinga dhidi ya magonjwa
19 October 2026, 16:46

Wananchi hao wameiomba Serikali na mamlaka husika kuendelea kutoa elimu na hamasa kuhusu utunzaji wa mazingira, huku wakitaka sheria zilizopo zisimamiwe na hatua stahiki zichukuliwe dhidi ya wanaokiuka taratibu za usafi na kusababisha uchafuzi wa mazingira.
Na Daniel Njau.
Usafi wa mazingira ni nguzo muhimu katika kulinda afya ya binadamu, lakini tabia ya baadhi ya watu kutofuata taratibu za utunzaji wa mazingira imeendelea kuwa changamoto inayoweza kuchangia kuenea kwa magonjwa yanayotokana na uchafu, hali inayozua wito wa kuimarisha uwajibikaji wa kila mmoja katika kudumisha usafi wa mazingira.
Baadhi ya wananchi wamesema uchafu wa mazingira unatokana na kutowajibika kwa baadhi ya watu, wakisisitiza kuwa juhudi za kuweka mazingira safi zinapaswa kuanzia kwa mtu binafsi na kuenea katika jamii ili kupunguza hatari ya magonjwa ya mlipuko.
Kwa upande wake, mtaalamu wa afya Bi. Magdalena Mgaya, amesema mazingira machafu na usafi duni wa mwili vinaweza kuchangia kuenea kwa magonjwa mbalimbali, yakiwemo magonjwa ya tumbo, akisisitiza umuhimu wa kunawa mikono kwa usahihi, hasa kwa watoto, kama njia mojawapo ya kujikinga na maambukizi.