Dodoma FM

Changamoto ya afya ya akili yatajwa sababu ya mtu kijitoa uhai

27 August 2026, 17:20

Matatizo ya afya ya akili yanaweza kupelekea mtu kushindwa kutimiza malengo yake na kutaka kujiua. Picha na mtandao.

Wananchi wameomba elimu ya afya ya akili na msaada wa kisaikolojia iendelee kutolewa vijijini na mijini ili kuongeza uelewa, kuimarisha ushirikiano wa jamii na kuwasaidia watu wenye changamoto kupata msaada mapema.

Na Daniel Njau

Hali ya baadhi ya watu kukata tamaa na kufikia hatua ya kutaka kujidhuru imeendelea kuwa changamoto katika jamii, huku wananchi wakihimizwa kutambua mapema dalili za msongo wa mawazo na kuwapatia wahusika msaada wa kisaikolojia na matumaini.

Mtaalamu wa saikolojia Dr Faustine China, amesema hali hiyo inaweza kuchangiwa na sababu za kisaikolojia, kijamii na kibaiolojia, huku baadhi ya dalili zikijumuisha hasira za mara kwa mara, kukata tamaa na mtu kueleza kuwa amechoka kuishi.

Amesema familia na jamii inayomzunguka mtu mwenye dalili hizo inapaswa kumsikiliza, kumtia moyo na kumsaidia kupata huduma stahiki badala ya kumtenga, kwani msaada wa mapema unaweza kuleta matumaini na kumsaidia kukabiliana na changamoto.

Sauti na Daniel Njau.