Dodoma FM

Senyamule ahamasisha ushiriki wa wazee katika uchaguzi

10 October 2025, 11:05 am

Picha ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamula katika kikao maalum kilichowakutanisha na wazee wa mkoa. Picha na Selemani Kodima.

Kikao hicho kimehitimishwa kwa maazimio ya pamoja ya kuimarisha ushirikiano kati ya viongozi wa serikali na wazee katika kuhakikisha mkoa wa Dodoma unakuwa mfano wa ushiriki wa kidemokrasia nchini.

Na Selemani Kodima.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mheshimiwa Rosemary Senyamule, ametoa wito kwa wazee wa mkoa huo kutumia kikamilifu haki yao ya kikatiba kwa kujitokeza kupiga kura katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29 mwaka huu.

Akizungumza katika kikao maalum kilichowakutanisha na wazee wa mkoa, Senyamule amesisitiza umuhimu wa wazee kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kidemokrasia, akieleza kuwa takwimu za awali zinaonyesha kiwango cha ushiriki wa wapiga kura katika mkoa wa Dodoma kilikuwa chini ikilinganishwa na idadi ya waliojiandikisha katika daftari la mpiga kura.

Sauti ya Mhe. Rosemary Senyamule.

Katika kikao hicho, baadhi ya wazee wameonesha moyo wa uzalendo kwa kumhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa wataendelea kuhamasisha jamii, hususan vijana na watu wa makundi mbalimbali, kushiriki kikamilifu katika uchaguzi huo muhimu.

Sauti za wazee.

Kikao hicho kimehitimishwa kwa maazimio ya pamoja ya kuimarisha ushirikiano kati ya viongozi wa serikali na wazee katika kuhakikisha mkoa wa Dodoma unakuwa mfano wa ushiriki wa kidemokrasia nchini.