Miradi 6 yenye thamani Bilion 1.6 yazinduliwa na mbio za mwenge Mpwapwa
1 June 2026, 17:20

Mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2026 zinabebwa na kaulimbiu isemayo Tanzania ni yetu sote tushikamane Kwa pamoja kuleta maendeleo.
Na Steven Noel.
Jumla ya miradi sita yenye thamani ya shilingi Bilion 1.6 imezinduliwa kutembelea na kuwekewa mawe ya Msingi na mwenge wa uhuru Kwa mwaka 2026 wilayani Mpwapwa.
Kiongozi wa mbio za mwenge mwaka 2026 Bwana Wazo Michael Mwang’onda amewataka watendaji wote wa serikali kutanguliza uzalendo mbele Ili miradi inayotolewa na serikali iweze kuwa na faida Kwa Wananchi wote .
Aidha ametumia fursa hiyo kuwahamasisha Wananchi wote kuweza kuendelea ,kulinda Amani ya Taifa kwa kuto kujihusisha kwenye vitendo vyovyote vinavyoweza kusababisha uvunjivu wa Amani.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Dkt Sophia Mfaume Kizigo amesema miradi hiyo iliyotembelewa na mbio za mwenge itakuwa chachu ya maendeleo Kwa wilaya hiyo Kwa mtu mmoja mmoja na Jamii Kwa jumla.